Posts

Showing posts from June, 2021

PAPA MSOFE AFUTIWA MASHTAKA, AACHIWA HURU

Image
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 18, 2021 imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne. Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo akieleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao. Msofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa wa mashtaka matano likiwemo la kujipatia Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu. Mbali na Papa Msofe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Wenceslaus Mtu(49), Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule (38) na Fadhil Mganga (61). Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa hao umetolewa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa DPP ameieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Baada ya upande mashtaka kueleza hiyo, Shaidi alikubaliana na o...

SERIKALI YATAKA WANAFUNZI WOTE KUSHIRIKI UMITASHUMTA

Image
  NAIBU Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo Mh Pauline Gekul akitoa hotuba ya kufunga Mashindano ya Umitashumta 2021 KIKUNDI cha Sanaa cha Mkoa wa Tanga kikitumbuiza kwenye Sherehe za ufungaji wa Mashindano ya Umitashumta leo mjini Mtwara ,Kikundi hicho kimeibuka na ushindi wa kwanza kwenye sanaa ya Ngoma Na John Mapepele, Mtwara Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (Mb) ameitaka  Kamati ya Kitaifa ya UMITASHUMTA na MISSETA kutoa muongozo wa kuhahikisha watoto wa Shule za Serikali na watu binafsi wanashiriki kikamilifu katika mashindano haya ili kujenga umoja, uzalendo na mshikamano kwa watoto wa Tanzania.   Mhe. Gekul ametoa kauli hiyo leo Juni 18, 2021 wakati akifunga mashindano ya UMITASHUMTA kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ambapo amesisitiza kuwa Malengo ya mashindano haya ni kutoa fursa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi kushiriki na kuonesha vipaji vyao vya michezo na sanaa walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu. “Kwa kupitia m...

RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA WILMAR INTERNATIONAL YA SINGAPORE

Image
 

UPELELEZI WA KESI MOJA KATI YA TANO ZINAZOMKABILI SABAYA WAKAMILIKA

Image
  Upelelezi wa kesi moja ya unyang'anyi wa kutumia silaha kati ya kesi tano zinazomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, umekamilika na kwamba ameanza kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo. Hayo yamejiri leo Juni 18, 2021, Jijini Arusha wakati kesi yake pamoja na wenzake  ilipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa ajili ya kutajwa tena kwa mara ya pili. Wakili mkuu wa Serikali,  Tumaini Kweka amemweleza hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya,  Salome Mshasha kuwa upande wa mashtaka umekamilisha upelelezi huo na upo tayari kuwasomea maelezo watuhumiwa. Mwendesha mashtaka wa Serikali,  Tarsila Gervas amesema Februari 9, 2021 katika mtaa wa Bondeni,   Sabaya akiwa na watuhumiwa wenzake wawili walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kuvamia duka la Said Saad na kuwaweka chini ya ulinzi. Gervas amesema Sabaya na walinzi wake,  Sylivester Nyingu (26) maarufu Kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa h...

RAIS WA KWANZA WA ZAMBIA K

Image
  Rais wa kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda amefariki dunia leo akiwa na miaka 97. Kenneth David Kaunda (anafahamika zaidi kama KK). Siku chache zilizopita, Dk. Kaunda alilazwa katika Hospitali ya Maina Soko jijini Lusaka kufuatia maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa siku kadhaa. Kaunda aliyezaliwa April 28, 1924, aliitawala Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991. Chanzo: BBC Swahili

Kilo 88 za dawa za kulevya zatelekezwa Ndani ya Prado Jijini Dar es Salaam

Image
  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imefanikiwa kukamata kilo 88.27 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine zikiwa ndani ya gari aina ya Toyota Prado iliyokuwa imetelekezwa barabarani. Akizungumza leo juni 17, 2021 jijini Dar es Salaam, Kamishina Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya amesema dawa hizo zimekamatwa Juni 2 mwaka huu, saa saba usiku katika eneo la Kimara Korogwe kwa ushirikiano wa DCEA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). "Baada ya upekuzi wa kisheria kufanyika ndani ya gari kulipatikana na mifuko mikubwa mitatu aina ya sandarusi (viroba), ndani yake ikiwa na pakti 12 za dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 12.25 pamoja na kontena za plastiki 73 ndani yake kukiwa na dawa aina ya Methaphetamine zenye uzito wa kilo 76.02," amesema Kamishina Jenerali Kusaya. Aidha, Kamishna huyo ameeleza kuwa upelelezi bado unaendelea ikiwemo kumgundua mwenye gari hilo na mtanadao wake kwani dereva wa gari hilo baada ya kugundua ...

Mwenge wa Uhuru kufungua na kukagua miradi 53 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 581 Jijini Arusha

Image
   Na Imma Msumba Mwenge wa Uhuru maalumu umeanza kukimbizwa katika mkoa wa Arusha ambapo utakapokuwa mkoani hapa utaweka mawe ya msingi,kuzindua, kufungua na kukagua miradi 53 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 581. Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amepokea Mwenge huo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere katika kijiji cha Kansay kilichopo wilaya ya Karatu. Mwenge wa Uhuru maalum umeanzia wilaya ya Karatu kwa kupita katika miradi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 3.4 Miongoni mwa miradi hiyo ni wa Ujenzi wa maabara katika kituo cha afya cha Endabash pamoja na mradi wa matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) . Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa Luteni Josephine Mwambashi akapokea taarifa,akakagua na hatima kufungua au kuzindua mara baada ya kutoa maeleko ya namna bora ya kuboresha miradi hiyo Mwenge huo utakuwepo katika mkoa wa Arusha kwa siku sita katika wilaya sita ukikimbizwa kwa jumla ya kilometa 950.35 Habar...

Waziri Mkuu Atoa Wito Kwa Taasisi Zinazoomba Misamaha Ya Kodi

Image
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zinazoomba misamaha ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini zifuate taratibu ikiwa ni pamoja na kueleza kikamilifu ni bidhaa gani wanayotaka kuileta nchini ili ipate msamaha huo na lazima ikidhi matakwa ya Serikali ikiwemo ya kwenda kutoa huduma iliyokusudiwa. Ametoa wito huo leo (Alhamisi, Juni 17, 2021) wakati akijibu swali la mbunge wa Kilolo Justine Nyamoga katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma. Mbunge huyo alitaka kufahamu Serikali imeweka utaratibu gani wa kutoa misamaha kwa baadhi ya taasisi za dini zinazotoa huduma kwa jamii. Mbunge huyo amesema taasisi za dini zimekuwa zikikumbwa na urasimu mwingi wakati wa kutoa vifaa au misaada mbalimbali kutoka nje ya nchi hali inayosababisha wakati mwingine vifaa hivyo kukaa muda mrefu bandarini na hatimaye kulazimika kulipia gharama za uhifadhi wakati wanatoa. Alihoji, nini kauli ya Serikali kuhusu tatizo hilo? Waziri Mkuu amesema Serikal...

Makamu Wa Rais Aiagiza Wizara Kuangalia Upya Masharti Kuasili Wa Mtoto

Image
  Na Mwandishi Wetu Dodoma Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango ameishauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, kupitia upya masharti ya utaratibu  wa kuasili watoto  ili kuhamasisha watanzania na watu wengine wenye nia njema  kuasili watoto hivyo kupunguza idadi ya watoto kwenye makao. Akizungumza June 16, 2021 wakati wa uzinduzi wa Makao ya Taifa ya watoto katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma, Makamu wa Rais ameiomba Wizara hiyo kupitia upya utaratibu huo ili kuwapa nafasi watanzania kuasili watoto ambao wanaishi kwenye makao hayo. "Naomba kutumia fura hii kuishauri Wizara kupitia upya masharti ya utaratibu wa kuasili watoto ili kuhamasisha watanzania na watu wengine wenye nia njema kuasili watoto hivyo kupunguza idadi ya watoto kwenye makao,"amesema Dkt. Mpango. Hata hivyo, Dkt.Mpango amewasihi watanzania wenye uwezo kuguswa na maisha ya watoto wanaishi kwenye mazingira hatarishi na wachukue hatua kuasili watot...

UJENZI NA UKARABATI WA MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WAANZA MADIBILA

Image
  Kulia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali Akimkabidhi Mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu katika Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Madibila Bw. David Noble Mkurugenzi wa Kampuni ya Ukandarasi ya White City International. Bw. Shabani Sawasawa (mkulima) akizungumzia manufaa ya Mradi wa Regrow katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji ya Madibila, iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali.   ·        ·         MKANDARASI AKABIDHIWA KAZI ·      >   LENGO NI KUKUZA UTALII NA UCHUMI KWA KANDA YA KUSINI   Na: MwandishiWetu – Madibila Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji katika skimu ya Madibila iliyopo katika Halmashauri ya Mbarali Mkoani Mbeya, umeanza rasmi kwa mkandarasi kukabidhiwa eneo la ujenzi wa mradi na mkataba kwa  utekelezaji wa mradi huo, ambao unalengo la kusimamia ustahimilivu wa maliasili kwa ajili ya ukuaji wa utal...

MIMBA ZA UTOTONI, UBAKAJI VIKWAZO VINAVYOWAKABILI WATOTO WA KIKE WILAYANI MKINGA

Image
    KAIMU Mkuu wa wilaya ya Mkinga Erick Farahani ambaye ni Afisa Tawala wa wilaya ya Mkinga akizungumza wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa lililofanyika wilayani humo Mwakilishi wa Wordvision Tanzania ,Agatha Matumaini akizungumza wakati wa Kongamano hilo Kaimu Afisa Elimu Sekondari Ajari Mwarimwengu akizungumza wakati wa kongamano hilo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga akizungumza wakati wa Kongamano hilo Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Mkinga Sosten Mtena akizungumza wakati wa Kongamano la siku ya Mtoto wa Africa 2021 lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo. SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo SEHEMU ya wanafunzi wakiwa kwenye Kongamano hilo SEHEMU ya wanafunzi wakiandamana wakati kongamano hilo MIMBA za Utotoni, Ubakaji, Ulawiti na ukosefu wa elimu ya jinsi ya afya na uzazi ni miongoni mwa vikwazo vinavyowakabili wato...