LUGHA 5 ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO (THE FIVE LOVE LANGUAGES)
Katika utafiti uliofanywa na Gary Chapman katika kitabu chake cha THE FIVE LOVE LANGUAGESii cha mwaka (1995) Anaeleza kuwa.... Katika maisha ya mahusiano, kila binadamu ana lugha yake ya mawasiliano katika mahusiano. Unagundua lugha ya mpenzi wako katika mahusiano kupitia kujua ni vitu gani au mambo gani anapenda kufanya kwako, na yeye anafurahia ikiwa utamfanyia.... Zifuatazo ni lugha 5 za mawasiliano katika mahusiano zilizofanyiwa utafiti na (Gary Chapman).... 1️⃣ Lugha ya maneno ya hamasa au uthibitisho. 〰️ Katika mahusiano kuna aina ya mtu anaetumia lugha hii ya mawasiliano katika mahusiano yake.Yeye hutoa maneno ya hamasa na hupenda kupokea maneno ya hamasa pia. Anapenda kusikia maneno ya shukrani, kupongezwa, kujali na kusifiwa ikiwa amefanya jambo fulani katika maisha yake. Aina hii ya mtu asipopata neno la hamasa au uthibitisho kutoka kwako basi ataliomba yeye mwenyewe ili alisik...