Kongamano Kongamano Kongamano
Chuo kikuu Cha Mtakatifu Augostino kilichopo malimbe jijini Mwanza kinawatangazia wanafunzi wake kuwa kutakuwa na kongamano la mafunzo juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu chuoni hapo siku ya Jumanne tarehe 8/11/2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika ukumbi wa M15.
Kongamano hilo limebebwa na kauli mbiu isemayo
"Matumizi Salama ya Mitandao na Maisha Mapya ya Wanafunzi SAUT”Kongamano hilo limeandaliwa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) wakishirikiana na uongozi Saint Augustine University of Tanzania(SAUT-Mwanza).Kongamano hili ni maalum kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu hususani mwaka wa kwanza ambao ndiyo wanaanza safari yao ya masomo ya Shahada mbalimbali za Elimu ya Juu.
Comments