Amuuwa mke wake na kujaribu kujiua kisa wivu wa mapenzi
Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nehemia Mohamed kabuta (40) ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe aliyefahamika kwa jina la Adela Ndihabati (40) kwa kumkata mapanga na kumtenganisha kiwiliwili na viungo vingine.
Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Aidha kamanda huyo wa polisi bwana James Manyama amesema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuwaona polisi alijaribu kujichinja na kitu chenye ncha kali ingawa hakuweza kufanikiwa kujiuwa kwani polisi walimuwahi na kumnyang'anya kitu hicho.
Kwa sasa mtuhumiwa huyo yupo hospitali na akipona atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Comments