Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nehemia Mohamed kabuta (40) ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe aliyefahamika kwa jina la Adela Ndihabati (40) kwa kumkata mapanga na kumtenganisha kiwiliwili na viungo vingine. Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Aidha kamanda huyo wa polisi bwana James Manyama amesema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuwaona polisi alijaribu kujichinja na kitu chenye ncha kali ingawa hakuweza kufanikiwa kujiuwa kwani polisi walimuwahi na kumnyang'anya kitu hicho. Kwa sasa mtuhumiwa huyo yupo hospitali na akipona atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 18, 2021 imemfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne. Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo akieleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao. Msofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa wa mashtaka matano likiwemo la kujipatia Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu. Mbali na Papa Msofe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Wenceslaus Mtu(49), Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule (38) na Fadhil Mganga (61). Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa hao umetolewa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa DPP ameieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Baada ya upande mashtaka kueleza hiyo, Shaidi alikubaliana na o...
Prof. Issa Shivji Kufuatia suala la wamasai kuhamishwa katika eneo la hifadhi ya ngorongoro Prof. Issa Shivji amemuandikia Rais Samia barua ya Wazi huku akieleza na kufafanua Sheria ya Ardhi. Pia amehitimisha kwa kusema Watu wa Ngorongoro na Loliondo hawawezi kuhamishwa bila kufuata taratibu za Kisheria na kwa sababu Mahususi itakayo wekwa wazi na Kujadiliwa. "Bila uhuru hakuna maendeleo. Bila maendeleo hakuna uhuru. Maendeleo ya kulazimishwa ni udikteta. Maendeleo ya hiari ni demokrasia." Prof. Issa Shivji Written by Rafael Masau
Comments