MFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB ANUSURIKA KUFA KWA KUPIGWA,KUKATWA MKONO SHINYANGA
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤:
Picha haihusiani na habari hapa chini
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Debora Rwekwama (34) mkazi wa Bushushu Mjini Shinyanga amenusurika kufa baada kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kukatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35) kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 usiku katika mtaa wa Bushushu, Manispaa ya Shinyanga.
“Debora Rwekwama (34) Banker - CRDB, mkazi wa Bushushu Manispaa ya Shinyanga alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya kupoteza fahamu alikatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35)mkazi wa Bushushu”,amesema Kamanda Kyando.
Ameeleza kuwa hali ya majeruhi ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama.
Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi na kwamba tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa wa tukio hilo.
Comments