Amuuwa bosi na watoto wake kisa kugombezwa

 Jeshi la polisi kanda maalumu ya dar es salaam limesema kuwa linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la shedrack Kapanga (13), ambaye alikuwa ni msaidizi wa kazi za ndani kwa tuhuma ya kumuua bosi wake na watoto wake wawili kwa madai ya kwamba amekuwa akigombezwa mara kwa mara.

Taarifa hiyo ilitolewa jana JUNI 12, 2021 na kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Muliro Jumanne wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 9, 202, maeneo ya masaki jijini Dar es salaam na mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 11, 2021, maeneo ya Magomeni akiwa kwenye harakati za kutoroka.

Waliofariki ni Emmy Mutaboyerwa ambaye ni Mama na mabinti zake wawili Daniela na Danita Mutaboyerwa.

Kamanda wa polisi kanda hiyo Bwana Muliro Jumanne amelaani kitendo hicho kilichofanywa na huyo kijana na kudai kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka hayo yanayomkabili.

Comments

Popular posts from this blog

PAPA MSOFE AFUTIWA MASHTAKA, AACHIWA HURU

The Ugandan Mixed School Where Boys Wear 'Skirts'