Hija 2021. Ni wakazi wa Saudi Arabia watakaofanya hija mwaka huu
Maafisa nchini Saudi Arabia wamesema ni watu 60,000 tu watakaoruhusiwa kufanya Hija, kulingana na wavuti wa Haramain Sharifain, ambao unaripoti kutoka katika misikiti miwili mitakatifu.
Aidha taarifa hiyo inasema ni wakazi wa Saudi Arabia pekee watakaoruhusiwa kufanya Hija mwaka huu, wakiwemo wageni wanaoishi nchini humo.
Wavuti huo unasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kusambaa kwa aina mpya ya virusi vya corona kote duniani.
Mwaka jana pia Saudi Arabia ilipiga marufuku watu wanaotoka mataifa mengine kufanya ibada ya Hija nchini humo ili kudhibiti virusi vya corona.
Watu takribani milioni 2, vinginevyo wangetembelea Maka na Madina kwaajili ya Hija hiyo inayofanyika kila mwaka kulingana na imani ya kiislamu.
Kumekuwa na hofu kwamba Hija inaweza kufutwa kabisa.
Kwa kawaida Hija ni moja ya vipindi muhimu sana katika kalenda ya watu wa kiislamu. Lakini ni raia wa nchi nyingine ambao tayari ni wakazi wa Saud Arabia ndio watakao ruhusiwa kuhudhuria Hija ya mwaka huu.
Maafisa nchini humo wanasema "hii ndiyo njia pekee itakayowezesha kufanya mipango ya watu kutokaribiana ambayo itawezesha watu wawe salama.
Saudi Arabia imerekodi visa vya corona 161,005 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo ni 1,307.
Comments