Profesa Mwasiga Baregu afariki dunia
Mwanasiasa wa chadema na mwanazuoni profesa Mwesiga Baregu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Profesa Baregu alikuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa na utawala wa umma chuo kikuu cha Dar es salaam, baadaye alisitishiwa mkataba wake kutokana na kinachoelezwa kuchanganya utumishi na siasa.
Baadaye profesa Baregu alihamia katika chuo kikuu cha mtakatifu Augustine (SAUT) Mwanza.
Lakini bwana Baregu baadaye alikuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA.
R.I.P Prf. Baregu
Comments