Rais wa Zambia azirai wakati wa kumbukumbu ya jeshi

 

  • Rais Edgar Chagwa Lungu alikuwa buheri wa afya Jumapili, Juni 13, wakati aliongoza hafla ya kumbukumbu ya 45 ya Jeshi la Ulinzi la Zambia.

  • Hata hivyo, akiwa katika hafla hiyo ya jeshi, rais huyo anadaiwa kuhisi kisunzi ghafla na kumpelekea kuzirai.

  • Alipata fahamu haraka na kuelekea moja kwa moja kwenye gari lake na kurejea Ikulu ambapo amekuwa akikagua vidimbwi vya samaki

  • Ripoti kutoka Zambia zinadai kuwa rais wa taifa hilo Edgar Chawga alizirai Jumapili, Juni 13, akiongoza hafla ya kumbukumbu ya 45 ya Jeshi la Ulinzi jijini Lusaka

Ripoti kutoka Zambia zinadai kuwa rais wa taifa hilo Edgar Chawga alizirai Jumapili, Juni 13, akiongoza hafla ya kumbukumbu ya 45 ya Jeshi la Ulinzi jijini Lusaka.

Rais wa Zambia Edgar Lungu Azirai Wakati wa Sherehe ya Kumbukumbu ya jeshi


Taarifa ya Waziri Simon Miti ilidai kuwa rais huyo alikumbana na kisunzi wakati wa hafla hiyo lakini alipata fahamu haraka na kuelekea moja kwa moja kwenye gari lake na kurejea Ikulu.

Miti alibainisha kuwa kiongozi huyo yuko katika hali nzuri na anaendelea kuchapa kazi.

Kupitia Miti, rais huyo aliwahakikishia raia wa Zambia na mashirika ya kimataifa kwamba yuko sawa na anaendelea na ratiba ya shughuli zake kama ilivyokuwa imepangwa.

Baada ya udukuzi kwenye ukurasa wake wa Facebook, TUKO.co.ke ilitambua rais huyo akionyeshwa mubashara kutoka Ikulu akikagua vidimbwi vya samaki.



Comments

Popular posts from this blog

PAPA MSOFE AFUTIWA MASHTAKA, AACHIWA HURU

The Ugandan Mixed School Where Boys Wear 'Skirts'