MFANYABIASHARA MAARUFU WA MADINI YA TANZANITE NA MMILIKI WA GOLD CREST HOTEL AFARIKI DUNIA

21 hours ago

Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Mathias Manga aliyekuwa anamiliki mgodi wa Tanzanite wa Manga Gems uliopo kitalu D amefariki dunia leo Alhamisi Agosti 12,2021 akiendelea kupatiwa matibabu nchini Afrika Kusini.

Manga pia alikuwa Mmiliki wa Hoteli za Gold Crest zilizopo jijini Arusha na Mwanza na alikuwa anamiliki majumba kadhaa ya kifahari jijini Arusha na amewahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (Tamida), Sammy Mollel amesema amepata taarifa za msiba wa Manga.

R.I.P Mathias Manga

Comments

Popular posts from this blog

PAPA MSOFE AFUTIWA MASHTAKA, AACHIWA HURU

The Ugandan Mixed School Where Boys Wear 'Skirts'