Picha & Video : WAFANYAKAZI WA TANESCO WAZUA GUMZO WAKIFYEKA SHAMBA LA MAHINDI TINDE

𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤:

Jana Alhamis Agosti 19,2021 kuna video imesambaa mtandaoni ikiwaonesha wafanyakazi wa TANESCO wakikata mahindi yaliyolimwa na mwananchi aliyejulikana kwa jina la Hemed Rashid katika eneo la Tinde wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Inaelezwa kuwa mahindi hayo yamelimwa kwenye njia kuu ya umeme.

Wakazi wa Tinde na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahoji :
"Hii ni halali ? Kwanini tunarudishana nyuma namna hii? Hii Tinde pata picha huyu mkulima  amelima TANESCO wakiwa wamemtazama Ila leo wameamua kuja kukata mimea hivi mnadhani mwananchi atawaelewaje? Haya mahindi yana athiri nini kwenye nguzo ? Kuna mimea ya tikiti nayo imekatwa madhara ya hiyo mimea 362 ya tikiti ni yapi?".

"Tunaomba mamlaka kutusaidia kwani kitendo hiki ni ukatili dhidi ya binadamu maswali hayana majibu, Je shamba hili lilimwa siku moja na kupandwa kisha mazao kukua kwa kasi? Je Mamlaka ya Tanesco haikuwahi kufika hapo tangu shamba linalimwa hadi mazao yalipochanua kiasi hicho ndipo wakayaona?

 Na je kwa  kwa kuwa yalikuwa yamelimwa na kuchanua kiasi hicho kile kinachoitwa taratibu  zingine ukiacha Sheria na kanuni zilishindwa kufanyika na kuonya? au yalikuwa maksudi ya kufanywa  ukatili huo ndiyo maana mahindi yakaachwa yapendeze ndipo yafyekwe? Bado tunajiuliza tukisubiri taarifa za kimamlaka", wameendelea kuhoji watumiaji wa mitandao ya kijamii walioona video clip hiyo.


Tazama picha na video zikionesha mimea hiyo ikikatwa
Mahindi yakikatwa
Mahindi yakikatwa
Miche ya matikiti ikiondolewa

Comments

Popular posts from this blog

Kauli ya Serikali Kuhusu Bei ya Mafuta

INASIKITISHA!! MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK September 22,2021

The ancients said that the way you feed a child is the way he/she grow up.