Posts

Showing posts from September, 2021

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 22,2021

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩:

INASIKITISHA!! MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK September 22,2021

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩: INASIKITISHA SANA! Matukio mengine ukimwambia mtu si rahihi kumuingia akilini, imagine mtu anapoteza watoto wake wapendwa tena mapacha eti kisa yuko live kwenye mitandao ya kijamii, like seriously? Watoto wawili mapacha wamefariki dunia mara baada ya kuporomoka kutoka ghorofa ya kumi wakati mama yao akiwa amezama LIVE katika mtandao wa Facebook. Mapacha hao ambao ni Moise Petrice wa kiume na Beatrice Petrice pacha wa kike wamekumbwa na umauti huo baada ya kudandia katika dirisha lililokuwa limeachwa wazi. Tukio hili limejitokeza katika jiji la Ploiesti nchini Romania. Polisi wamethibitisha kwamba mama wa watoto hao hakugundua kama wanae wameporomoka na kufariki dunia hadi hapo aliposikia milio ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) huku kukiwa na mtu akibisha hodi mlangoni kwake. Muda wote huo mpaka watoto wanafariki yeye alikuwa bize LIVE Facebook akiongea na wafuasi wanaomfuatilia katika ukurasa wake wa mtandao huo wa facebook. I...

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUIBUA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩: Na  Frankius Cleophace Mara.  Katika kuelekea  siku ya kimataifa ya amani  waandishi wa Habari  Mkoani Mara wameaswa kuendelea kuibua habari zinazohusu watoto wadogo kuanzia umri wa miaka sifuri hadi nane ili waweze kukua na kupata malezi bora.  Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani  Mara Raphael Okello  wakati wa mahojiano  maalum kuelekea kilele cha  siku ya amani Kimataifa ambapo nchini Tanzania maadhimisho hayo kilele chake kilifanyika Jijini Dodoma september 21,2021 Okelo alisema kuwa watoto wamekuwa wakitelekezwa na wazazi wao hivyo sasa ni jukumu la waandishi wa habari kuendelea kuibua habari hizo na changamoto ili ziweze kutatuliwa mapema.  “Tunazungumzia suala la Amani, amani hawezi kuwepo wakati watoto wadogo wasiokuwa na hatia wanazaliwa wanatelekezwa hivyo sasa waandishi wa habari tukiungana na serikali katika kuibua masuala hayo ...

WAUMINI WAPIGANA LIVE KANISANI 7 minutes ago

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩: Mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya vurugu kuzuka wakati wa ibada katika kanisa la Kenya Assemblies of God, (KAG) eneo la Sagana kaunti ya Kirinyaga Jumapili, Septemba 19,2021 Imeripotiwa kwamba waumini walitaka Askofu Ben Irungu wa eneo la Mlima Kenya kuwatangazia mhubiri wao mpya ikizingatiwa wa awali alifariki dunia mwezi Machi mwaka huu.  " Askofu, kabla ukamilishe ibada, tunafahamu leo ni siku kuu kwetu sisi kwa sababu unamtambulisha mhubiri mpya kufuatia kifo cha Mhubiri wa awali William Wachira ambaye aliaga dunia mwezi Machi mwaka huu," Muumini mmoja aliyetambulika kama Francis Gachau aliuliza.  Waumini walimuidhinisha Mchungaji Esther Wachira ambaye alikuwa mkewe marehemu mchungaji Wachira. “Huyu mama alianza kanisa na mume wake, sasa wakati Kanisa imesimama wanataka kupatia mtu mwingine uongozi wa kanisa, hatutakubali hilo,” Baadhi ya waumini walisema.  Waumini walimkashifu Askofu Irungu kwa kupendekeza mhubi...

DKT. NDUGULILE AKABIDHI RASMI OFISI YA WIZARA KWA WAZIRI MPYA DKT. KIJAJI 2 hours ago

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩: Prisca Ulomi na Faraja Mpina, Dodoma Mbunge wa Kigamboni na aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile leo tarehe 20.09.2021 amekabidhi rasmi Ofisi kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa fursa ya kuhudumu katika Wizara hiyo katika kipindi cha miezi sita ya Serikali ya Awamu ya Sita Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Menejimenti ya Wizara hiyo Dkt. Ndugulile amempongeza Dkt. Kijaji kwa kuteuliwa na kuapishwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo na kumzungumzia kuwa ni kiongozi makini, mwenye uwezo mkubwa na anaamini atakuwa na mchango mkubwa katika Sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA Aidha, Dkt. Ndugulile ameishukuru Menejimenti ya Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika kufanya kazi ya kuijenga Wizara hiyo na hatimaye kuongezewa majukumu mengine huku akiy...

WAZIRI MKUU AKATAA KUFUNGUA OFISI YA TANESCO KYERWA September 20,2021

Image
𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekataa kuzindua mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kwa sababu gharama zilizotumika ni kubwa kuliko aina na idadi ya majengo yaliyopo. “Nikiweka jiwe la msingi nitakuwa nimehalalisha majengo mengine yajengwe kwa gharama hii. Siwezi kuweka jiwe la msingi, gharama zilizotumika ni kubwa kuliko majengo yaliyopo. Simamieni ujenzi wa majengo yenu na mjenge kwa kutumia mfumo wa force account.” Mheshimiwa Majaliwa amekataa kufungua ofisi hiyo leo (Jumatatu, Septemba 20, 2021) wakati akiwa katika katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo. “Nini kilisababisha hadi kibanda kigodo cha mlinzi kikajengwa kwa shilingi milioni saba? Kina matofali mangapi kama sio ulaji nini? hii si sahihi sijaweka jiwe la msingi wala kufungua na kile kibao kilichoandikwa jina langu kiondolewe. Serikali ipo makini katika usimam...

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 15,2021

Image
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤: Magazetini leo Jumatano September 15 2021

Yafahamu Matukio matano yaliyoitikisa Marekani 12, Septemba 2021

Image
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤: BBC News , S CHANZO CHA PICHA, Marekani ni taifa kubwa kiuchumi linalotajwa kuwa taifa namba moja duniani lenye nguvu ya ushawishi kwenye maeneo mengi ikiwemo kijeshi, kisiasa na kiuchumi. Mara nyingi limekuwa mstari wa mbele kwenye kuchukua hatua ama maaamuzi yenye kugusa jamii kubwa. Nguvu zake zimeifanya kuwa taifa lenye watu wengi wanaolipenda yakiwemo mataifa mbalimbali, lakini pia ni moja ya mataifa yanayochukiwa kutokana na maamuzi na wakati mwingine inavyotafsiriwa kuingilia utamaduni ama masuala ya nchi zingine. Pamoja na hilo na kuwa na nguvu hizo, taifa hilo limekuwa likipitia misukosuko mingi iliyotikisa historia yake na kuacha kumbukumbu isiyofutika. Baadhi ya matukio yasiyosahaulika kwa Wamarekani ni haya matano 5: Shambulio katika Ubalozi wa Marekani huko Tehran, Iran Katika miaka ya 1970 kuliibuka vuguvugu la kiutawala baada ya vijana wengi wa nchi hiyo kuupinga utawala wa Mohammed Reza Shah Pahlavi...

Wamarekani wawakumbuka waliopoteza maisha kwa shambulio la Septemba 11,2001) 11 Septemba 2021

Image
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤: BBC News , S CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Wakati  usomaji wa majina unaendelea, wacha tukumbuke uzoefu wa siku hiyo. Wakati ndege ilianguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa Kituo cha Biashara cha Dunia, Tom Canavan alikuwa kwenye ghorofa ya 47. Aliviambia vyombo vya habari kile kilichotokea siku hiyo. "Mimi na wenzangu tulishuka kwenye ngazi na tulikuwa tunakwenda chini. Nilirudi nyuma kusaidia wenza wazee kupitia milango. "Kisha jengo la kusini lilianguka na kifusi kilianguka juu yetu. Iliwaua wafanyakazi wenzangu ambao walikuwa wakitembea mbele yangu. "Sina hakika ikiwa nilipoteza fahamu, lakini wakati fulani, niliweza kutoka nje ya kifusi. Nilikuwa na bahati ya kutoka kwenye eneo la tukio nikiwa hai, kwa sababu ya kile kilichokuwa kikitupiga kutoka juu. Wakati ukiangalia picha za wingu hilo kwenye Runinga, hauoni kilicho kwenye vumbi hilo, lakini kwa kweli, moshi ulikuwa umejaa mashine za kunakili, komp...

Kauli ya Serikali Kuhusu Bei ya Mafuta

Image
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤: WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda timu maalumu ili kuchunguza kupanda kwa bei ya mafuta kwa kuwa kitendo hicho kinawaumiza wananchi hususan wale wa hali ya chini. Amesema Serikali imechukua uamuzi huo baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati nchini (EWURA) kutangaza bei mpya elekezi ya mafuta kwa mwezi Septemba ambapo ilionesha kupanda kwa bei za bidhaa hizo.  EWURA ilitangaza bei hiyo tarehe 31 Agosti, 2021. Waziri Mkuu ametoa taarifa hiyo (Ijumaa, Septemba 10, 2021) wakati wa kuahirisha Mkutano wa Nne wa Bunge la 12 jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 2 Novemba, 2021. Amesema kufuatia tangazo hilo la kupanda kwa bei za bidhaa hizo, Septemba Mosi, 2021, Serikali ilisitisha bei mpya zilizotangazwa na EWURA ili kufanya mapitio ya kina ya kupanda huko kwa bei na siku iliyofuata iliunda timu ya uchunguzi.

MFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB ANUSURIKA KUFA KWA KUPIGWA,KUKATWA MKONO SHINYANGA

Image
𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤: Picha haihusiani na habari hapa chini Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Debora Rwekwama (34) mkazi wa Bushushu Mjini Shinyanga amenusurika kufa baada kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kukatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35) kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 usiku katika mtaa wa Bushushu, Manispaa ya Shinyanga. “Debora Rwekwama (34) Banker - CRDB, mkazi wa Bushushu Manispaa ya Shinyanga alishambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na baada ya kupoteza fahamu alikatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35)mkazi wa Bushushu”, amesema Kamanda Kyando. Ameeleza kuwa hali ya majeruhi ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama. Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi na kwamba tayari Jeshi l...