Wamarekani wawakumbuka waliopoteza maisha kwa shambulio la Septemba 11,2001) 11 Septemba 2021
Wakati
"Mimi na wenzangu tulishuka kwenye ngazi na tulikuwa tunakwenda chini. Nilirudi nyuma kusaidia wenza wazee kupitia milango.
"Kisha jengo la kusini lilianguka na kifusi kilianguka juu yetu. Iliwaua wafanyakazi wenzangu ambao walikuwa wakitembea mbele yangu.
"Sina hakika ikiwa nilipoteza fahamu, lakini wakati fulani, niliweza kutoka nje ya kifusi. Nilikuwa na bahati ya kutoka kwenye eneo la tukio nikiwa hai, kwa sababu ya kile kilichokuwa kikitupiga kutoka juu.
Wakati ukiangalia picha za wingu hilo kwenye Runinga, hauoni kilicho kwenye vumbi hilo, lakini kwa kweli, moshi ulikuwa umejaa mashine za kunakili, kompyuta, simu, viti - na watu.
"Nilikuwa na bahati sana, kabla ya jengo la Kaskazini kushuka pia na nikapigwa tena na vifusi.
"Nilipelekwa hospitalini na niliweza kuzungumza na mke wangu kwa simu. Alikuwa mjamzito na binti yetu, na mtoto wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka mitatu tarehe 17 Septemba.
Wanafamilia wanasoma kwa sauti majina ya wapendwa wao. Ni wakati mgumu kwa wengine kuhimili.
Mike Low, ambaye alipoteza binti yake Sarah mnamo 11/9/ 2001, alianzisha usomaji huo.
Akiongea pole pole, kwa dhati, anawashukuru wale waliomsaidia yeye na familia yake, ambao "walitutoa katika siku zenye giza zaidi za maisha yetu".
Anatoa wito wa kuwa historia ya 11/9/2001 ikumbukwe, "sio kama nambari au tarehe, lakini sura za watu wa kawaida".
Ni kama jana
Wengi wanazungumza wakitokwa na machozi, sauti zinatetemeka. Hawa ni wakina mama, baba, wake, waume, wana na mabinti na wapwa
Kila mmoja pia ametoa maneno machache kwa ajili ya kumbukumbu.
Miaka ishirini inaonekana kama tukio la hivi karibuni.
Comments