WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUIBUA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO

𝙁𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬 𝙖𝙣𝙙 𝙖𝙙𝙙 𝙮𝙤𝙪𝙧 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩:


Na  Frankius Cleophace Mara.

 Katika kuelekea  siku ya kimataifa ya amani  waandishi wa Habari  Mkoani Mara wameaswa kuendelea kuibua habari zinazohusu watoto wadogo kuanzia umri wa miaka sifuri hadi nane ili waweze kukua na kupata malezi bora.

 Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani  Mara Raphael Okello  wakati wa mahojiano  maalum kuelekea kilele cha  siku ya amani Kimataifa ambapo nchini Tanzania maadhimisho hayo kilele chake kilifanyika Jijini Dodoma september 21,2021

Okelo alisema kuwa watoto wamekuwa wakitelekezwa na wazazi wao hivyo sasa ni jukumu la waandishi wa habari kuendelea kuibua habari hizo na changamoto ili ziweze kutatuliwa mapema.

 “Tunazungumzia suala la Amani, amani hawezi kuwepo wakati watoto wadogo wasiokuwa na hatia wanazaliwa wanatelekezwa hivyo sasa waandishi wa habari tukiungana na serikali katika kuibua masuala hayo na kutoa taarifa mapema ili watoto wapate malezi bora itasaidia kwa kiasi kikubwa”, alisema Okello.

 Vile vile Okello alisisitiza wazazi na walezi kuendelea kulinda na kulea watoto katika maadili mema ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule  watoto wote ili waweze kupata elimu bila kubagua hali zao.

“Kuna watoto pia ambao wanazaliwa na ulemavu hawapelekwi shule hivyo sasa jamii iungane kwa pamoja kwa lengo la kutoa haki  sawa” alisema Okello.

 Kwa upande wake Valerian Mgani kutoka shirika la ATFGM Masanga aliongeza kuwa suala la malezi na makuzi ni jukumu la wazazi wote hivyo kuelekea kilele cha siku ya amani wazazi waendelee kutoa malezi bora watoto wao.

“Pia nasisitiza  watanzania kuendelea kudumisha suala la amani ili kuendelea kutimiza majukumu yetu kwa sababu bila amani hakuna kitakachofanyika pia uchumi utuayumba”, alisema Valerian.

Maadhimisho ya siku ya amani kimatiafa hufanyika September 21  kila mwaka ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema kuwa  "Kujikwamua zaidi  katika dunia  yenye usawa  zaidi"

Comments

Popular posts from this blog

Kauli ya Serikali Kuhusu Bei ya Mafuta

INASIKITISHA!! MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK September 22,2021

The ancients said that the way you feed a child is the way he/she grow up.