Amuua jirani yake aliyemtuhumu kuwa anamloga TUESDAY SEPTEMBER 07 2021

𝙪𝙨𝙞𝙨𝙖𝙝𝙖𝙪 𝙛𝙤𝙡𝙡𝙤𝙬, 𝙣𝙖 𝙩𝙤𝙖 𝙘𝙤𝙢𝙢𝙚𝙣𝙩 𝙮𝙖𝙠𝙤:
jirani pc


Babati. Mkazi wa Kijiji cha Mutuka Wilayani Babati Mkoani Manyara, Samson Daudi (26) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua Peter Buu (48) akimhusisha na imani za kishirikina.


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Grafton Mushi amesema leo Septemba 7, 2021 kuwa tukio hilo limetokea juzi kwenye kijiji hicho baada ya Daudi kumtuhumu Buu anamloga ili nyumba yake isimalizike kujengwa.


Mushi amesema mtuhumiwa alimuua Buu kwa kumkata mara tatu shingoni kwa kutumia panga na kisha akafariki dunia papo hapo.


"Mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu kufanya ushirikina na kukwamisha ujenzi wa nyumba yake ambayo imeshindikana kukamilika," amesema Mushi.


Amesema kabla ya tukio hilo marehemu alifika shambani mwa mtuhumiwa aliyekuwa akimtuhumu kukwamisha ujenzi wa nyumba yake kwa kumroga na ndipo ugomvi uliibuka na Daudi akaanza kumwambia kuwa anamuroga ili asimalize nyumba yake ndipo akaanza kumshambulia kwa mapanga.


Mushi amewataka wananchi kutafuta suluhu ya matatizo yao kwa kufikiria njia sahihi na siyo kwenda kwa waganga wa kienyeji ambao watawapotosha.

ADVERTISEMENT


"Nawaonya wananchi wanaoamini kishirikina kuacha mara moja ili kuepuka kufanya uharifu wa mauaji kama haya," amesema Mushi.


Amesema mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi unaendelea muda wowote atafikishwa mahakamani pindi ukikamilika.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Mutuka, Peter Yambi amesema matukio ya aina hiyo ya mauaji yalikuwa yanatokea miaka ya nyuma.
Amesema chanzo cha matukio ya namna hiyo ni vijana kunywa pombe na kutumia dawa za kulevya ambazo husababisha matukio ya kikatili.


Yambi amesema mtuhumiwa siyo mtu wa kudumu katika kijiji hicho kwa kuwa hutoka na kurudi hivyo ni vigumu kumjua vizuri tabia yake.

Comments

Popular posts from this blog

PAPA MSOFE AFUTIWA MASHTAKA, AACHIWA HURU

The Ugandan Mixed School Where Boys Wear 'Skirts'