Majanga Yaanza Simba CAF Yatuma Ujumbe Mzito
Shirikisho la soka Afrika, CAF limetoa orodha ya makocha ambao hawaruhusiwi kukaa kwenye benchi kwenye mechi za mashindano ya Klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, wanapaswa kukaa jukwaani.
Kwenye hiyo orodha yupo kocha wa klabu ya Simba Simba, Didier Gomes da Rosa ambaye atatakiwa kukaa jukwaani mechi za CAF Champions League.
CAF wanataka kocha mkuu awe na leseni ya UEFA A PRO ambayo ni sawa na CAF A.
Didier Gomez da Rosa ana leseni ya UEFA DIPLOMA A na inatakiwa ni UEFA DIPLOMA A PRO.
Vyama vya soka vinavyoongoza vilabu tajwa kwenye orodha (TFF ya Tanzania na FERWAFA ya Rwanda) vimeshapewa taarifa mapema.
Comments