Namna unavyoweza kuishi katika Ulimwengu wa wakatishaji tamaa
𝐅𝐎𝐋𝐋𝐎𝐖 𝐏𝐀𝐆𝐄 𝐍𝐀 𝐓𝐎𝐀 𝐂𝐎𝐌𝐌𝐄𝐍𝐓 𝐘𝐀𝐊𝐎 𝐇𝐀𝐏𝐎 𝐂𝐇𝐈𝐍𝐈👇👇
Dunia ya leo imejaa maneno mengi kuliko watu waliopo katika dnia hiyo. Hebu fikiria ya kwamba tafiti za wanasaikolojia zinasema ya kwamba, mwanaume huzungumza maneno 16000 kwa siku, wakati wanaweke wote duniani kwa kila mmoja mmoja huzungumza maneno 25000 kwa siku, kwa tafiti hizi najaribu kuwaza hivi tuna watu wangapi? Na kila mmoja akizungumza maneno yake tutakuwa na maneno mangapi?
Najaribu tu kuwaza kwa sauti ili ujue ni kwa jinsi gani maneno yalivyozidi idadi ya watu. Nasema hayo kwa sababu katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukiishi katika ulimwengu wa kusema na kusikia. Na katika kusema wapo wale ambao huzungumza mambo chanya na wapo wale ambao huzungumza mambo hasi. Na katika kusikia ipo hivyohivyo sawa na kusema.
Hata hivyo maneno ya watu ambayo yapo katika dunia hii ni yale ambayo yanatengeneza ulimwengu mpya, ulimwengu huo huitwa ulimwengu wa taarifa, katika ulimwengu huo yapo mengi ambayo utayasema na mengine utayasikia, na katika ulimwengu huohuo tarifa hizo hizo ambazo utakuwa unazisikia, yapo yale yatakayokujenga, lakini yapo yale ambayo yatakufanya uvurugike kabisa.
Na ukweli ni kwamba maneno ya watu ni sumu, maneno ya watu yana nguvu sana kuliko nguvu za Samson hii ni kwa mujibu ya wahenga wapya. Uhalisia ulipo katika sayari hii ya kupeana taarifa zimejaa tarifa za kukatishana tamaa kuliko kupeana mbinu za kusonga mbele kimaisha.
Na mara kadhaa hali hii hutokea na unaweza ukajikuta unaumia sana kwenye maisha yako, hiyo yote kwa sababu ya maoni hasi ya watu wanayokutolea wewe. Sasa ili usiendelea kuumia kwa jambo hilo, kumbuka hivi, hicho ambacho kinaongelewa juu yako ni kwa mujibu wa maoni yao wao wenyewe ila uhalisia wa wewe jinsi ulivyo unaujua wewe.
Hivyo, tunachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba acha kuchukua maoni ya watu na ukaamua kuyatumia kuendesha maisha yako, kwa sababu kama ukifanya hivyo utamuia sana na utaiona dunia chungu. Hivyo ni vyema ukaamua kuishi wewe kama wewe kwa kufata kile ambacho moyo wako unakutuma kukufanya. Kufanya hivyo itakufanya uishi maisha ya ushindi na mafanikio makubwa.
Tumalizie kwa sema ya kwamba endapo utamua kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwasiliza wakatishaji tamaa katika dunia hii, kutakufanya uishi maisha ya ushindi siku zote za maisha yako. Lakini pia faida nyingine ambazo utazipata pale ambapo utamua kuishi maisha ya kujitolea hukumu, utakuwa na uhuru mkubwa katika kutoa maamuzi yako.
Asante sana kwa kuwa nasi, tunakutakia siku njema na mafanikio mema.
Imeandikwa na;
Imani Ngwangwalu & Benson Chonya
Comments