Jeshi la polisi mkoani Kigoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nehemia Mohamed kabuta (40) ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe aliyefahamika kwa jina la Adela Ndihabati (40) kwa kumkata mapanga na kumtenganisha kiwiliwili na viungo vingine. Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama ameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Aidha kamanda huyo wa polisi bwana James Manyama amesema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuwaona polisi alijaribu kujichinja na kitu chenye ncha kali ingawa hakuweza kufanikiwa kujiuwa kwani polisi walimuwahi na kumnyang'anya kitu hicho. Kwa sasa mtuhumiwa huyo yupo hospitali na akipona atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
TAZAMA BEI MPYA HAPA Tuesday, November 01, 2022 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, bezi hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Novemba 02, 2022 saa 6:01 usiku. EWURA NA RAFAEL MASAU
Prof. Issa Shivji Kufuatia suala la wamasai kuhamishwa katika eneo la hifadhi ya ngorongoro Prof. Issa Shivji amemuandikia Rais Samia barua ya Wazi huku akieleza na kufafanua Sheria ya Ardhi. Pia amehitimisha kwa kusema Watu wa Ngorongoro na Loliondo hawawezi kuhamishwa bila kufuata taratibu za Kisheria na kwa sababu Mahususi itakayo wekwa wazi na Kujadiliwa. "Bila uhuru hakuna maendeleo. Bila maendeleo hakuna uhuru. Maendeleo ya kulazimishwa ni udikteta. Maendeleo ya hiari ni demokrasia." Prof. Issa Shivji Written by Rafael Masau
Comments