Rais azindua Shamba la bangi la Mamilioni

Rais Emerson Mnangagwa katikati akiwa amezungukwa na jopo la Madaktari nchini Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amezindua shamba la bangi kwa ajili ya dawa lenye thamani ya dola za kimarekani milioni 27.

Shamba hilo limewekewa kiwanda cha kisasa cha usindikaji ambacho bangi yake itatumika kama suluhisho la matibabu ya kibaolojia na bidhaa za dawa katika soko la ndani na la kimataifa.

Mradi huu ni kwa ushirikiano na Serikali ya Uswizi kupitia kiwanda cha Swiss Bioceuticals na Serikali ya Zimbabwe.

Rais Mnagangwa amesema kuwa ushirikiano huo unaonyesha imani ya Uswizi katika kuwekeza ndani ya uchumi wa Zimbabwe huku akisema kuwa taifa hilo la Ulaya tayari limeshirikiana na Zimbambwe katika miradi mingine kama vile viwanda, usindikaji wa chakula na ujenzi wa taasisi mbalimbali.
Imeandaliwa na Rafael Masau

Comments

Popular posts from this blog

Kauli ya Serikali Kuhusu Bei ya Mafuta

INASIKITISHA!! MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK September 22,2021

The ancients said that the way you feed a child is the way he/she grow up.