Fahamu umuhimu wa uwepo wa mitandao ya kijamii na kusudi la maadhimisho yake kila ifikapo Juni 30.
Mitandao ya kijamii Pamoja na kuunganisha watu duniani kote, Mitandao imetoa fursa kwa watu kutengeneza kipato. Siku ya Mitandao ya Kijamii inaadhimishwa kusherehekea mahusiano ambayo watu wamejenga kupitia Mitandao mbalimbali. Uwepo wa Mitandao ya Kijamii umesaidia upatikanaji wa Taarifa, umetoa fursa kwa sauti za Wananchi kusikika na kuchochea Serikali duniani kote kutatua changamoto za Raia haraka zaidi. Mitandao ina nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko ikitumika vizuri. Je, unatumiaje nafasi yako katika Mitandao ya Kijamii? ULINZI WA FARAGHA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII Ili kujilinda unapotumia Mitandao mbalimbali ya Kijamii, inashauriwa; 1) Kuwa Makini na Taarifa zako binafsi: Ni muhimu kutoweka kila kitu Mitandaoni kwani baadhi ya taarifa zako zinaweza kutumiwa vibaya na kuleta madhara 2) Epuka kuweka kila kitu Mitandaoni: Kufanya hivi kunaweza kuweka Taarifa zako, angalia 'Privacy Setting' kujua namna unaweza kujiongezea usalama 3) Nenosiri (Password) Imara: Kuwa na Nenosiri ...